• HABARI MPYA

  Friday, October 05, 2018

  MKUU WA WILAYA PANGANI, ZAINAB ABDALLAH AMKABIDHI NTALE RAJAB BAJAJI YA SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya SportPesa imeendelea kukabidhi Bajaji kwa washindi ambao wametupia ubashiri na kuingia kwenye Droo ya Shinda Zaidi na SportPesa na wakati huu timu hii ya ushindi iliweka kambi Mwera wilaya ya Pangani mkoa wa Tanga .
  Hapa ilikuwa ni zamu ya mshindi wa Droo ya Kwanza kabisa Bwana Ntale Rajabu ambaye tayari amekabidhiwa bajaji yake zoezi ambalo lilisimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi, Zainab Abdallah 
  Akizungumza wakati wa kumkabidhi bajaji hiyo kutoka SportPesa mkuu wa wilaya `pangani Bi Abdallah alisema walikuwa wakiisikia SportPesa lakini kwa macho sasa ameshuhudia inavyobadili maisha ya watanzania baada ya kijana kutoka wilaya yake kushinda na hivyo kuwataka wananchi wa Pangani kucheza zaidi ili kupata washindi wengine zaidi.
  Mshindi wa kwanza wa promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa Ntale Rajabu akikabidhiwa bajaji na Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zainab Abdallah ,pembeni ni ndugu wa karibu wa Ntale.

  "Leo tunashuhudia kwa Macho Baada ya Ntale kuwa mshindi kutoka hapa pangani naomba Hii iwe hamasa kwa wengine zaidi kucheza kwa sababu unaposhinda bajaj hii kutoka SportPesa ndio Mwanzo wa kubadili maisha tunawashukuru sana SportPesa kufanya mambo haya kwa vitendo na kwa uwazi mkubwa " Alisema Bi Abdallah.
  Kwa upande mwingine mshindi wa bajaji hiyo ya Droo ya Kwanza ya Shinda Zaidi na SportPesa,  Ntale alishukuru sana kampuni hiyo ya michezo ya kubashiri hapa nchini kwa kueleza kuwa mwanzo hakuamini kabisa baada ya kuambiwa ameshinda lakini alipoona timu ya SportPesa imefika mpaka nyumbani kwao ikiongozwa na mkuu wa wilaya ndipo aliamini.
  "Namshukuru sana Mungu kweli SportPesa wamebadili maisha yangu naenda kuufungua ukurasa mpya katika maisha yangu naamini bajaji itakuwa msaada mkubwa kwangu na familia yangu kwa ujumla" Alisema Rajabu.
  Mama mzazi wa Rajabu nae anasema wakati mwanae anamwambia ameshinda na SportPesa hakuamini lakini baada ya kuiona Bajaji ndipo imani yake ilitimia na kuonyesha uso wa furaha kwa ushindi huo wa kijana wake 
  Hii ni Fursa kwa Watanzania kutoka SportPesa na hii inatokea pale unapoweka ubashiri wako na SportPesa moja kwa kwa moja unaingia kwenye droo ya Bajaj ni kwa kutumia simu yeyote ya  mkononi unapiga *150*87# au unacheza kupitia tovuti www.sportpesa.co.tz. kumbuka ili ucheze ni lazima uweke pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 unapocheza mara nyingi zaidi ndio unaongeza nafasi ya kushinda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKUU WA WILAYA PANGANI, ZAINAB ABDALLAH AMKABIDHI NTALE RAJAB BAJAJI YA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top