• HABARI MPYA

  Thursday, October 11, 2018

  KENYA WATOA SARE NA ETHIOPIA KUFUZU AFCON 2019

  KENYA imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji, Ethiopia katika mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku wa jana Uwanja wa Bahir Dar mjini Bahir Dar.
  Lakini ni sare ambayo wageni wangeweza hata kuibuka na ushindi kama wangetumia nafasi nyingi nzuri walizotengeneza.
  Na baada ya sare hiyo, timu zote zinafikisha pointi nne na sasa kuwa juu ya wapinzani wao wengine kwenye kundi hilo, Ghana na Sierra Leone watakaomenyana Jumatatu ambao wana pointi tatu kila mmoja.

  Mechi nyingine ya kufuzu AFCON ya mwakani iliyochezwa jana, Kundi K wenyeji Zambia wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea-Bissau Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola.
  Ushindi huo wa kwanza unawafanya Zambia wafikishe pointi nne baada ya kutoa sare moja na kufungwa mechi moja katika mbili za awali, sasa wakilingana na Guinea-Bissau iliyochea mechi tatu pia na Msumbiji ambayo hata hivyo imecheza mechi mbili.
  Namibia ambayo Jumamosi itawakaribisha Msumbiji ndiyo inashika mkia kwenye kundi hilo kwa pointi yake moja, amabyo nayo kama ikishinda keshokutwa timu zote zitakuwa na pointi nne baada ya mzunguko wa kwanza. 
  Mechi zaidi na kufuzu AFCON ya 2019 mwakani Cameroon zinaendelea leo hadi katikati ya wiki ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KENYA WATOA SARE NA ETHIOPIA KUFUZU AFCON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top