• HABARI MPYA

  Monday, October 08, 2018

  KAMATI YA SAA 72 YAMFUTIA ADHABU REFA ATHUMANI LAZI ALIYEFUNGIWA MIEZI MITATU KIMAKOSA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), maarufu kama Kamati ya Saa 72 imemuondolea adhabu ya kufungiwa miezi mitatu Mwamuzi Athumani Lazi baada ya kukubaliana na malalamiko yake kuwa jukumu la kuangalia off side katika mechi ni la Mwamuzi Msaidizi.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu baada ya kupokea malalamiko ya Lazi juu ya uamuzi wa Kamati kumfungia miezi mitatu kwa kosa Msaidizi wake, Nicholas Makaranga kunyoosha kibendera kukataa bao la Ruvu Shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji aliotea wakati hakuwa ameotea. 

  Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura (katikati) akiwa na Rais wa TFF, Wallace Karia

  Makaranga alifungiwa miezi sita kutokana na kitendo hicho katika mechi hiyo iliyofanyika Agosti 26, 2018 Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMATI YA SAA 72 YAMFUTIA ADHABU REFA ATHUMANI LAZI ALIYEFUNGIWA MIEZI MITATU KIMAKOSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top