• HABARI MPYA

  Wednesday, October 03, 2018

  JUMA ABDUL, AKILIMALI WAREJEA KUIONGEZEA NGUVU YANGA MECHI NA MBAO FC JUMAPILI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kulia wa Yanga SC, Juma Abdul Jaffar Mnyamani aliyekuwa majeruhi tangu mwezi uliopita leo ameanza mazoezi kikamilifu na wenzake baada ya kupona.
  Abdul aliumia Agosti 23 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu Yanga ikishinda 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar huku akitolewa dakika ya 89, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo Said Juma ‘Makapu’.
  Mchezaji huyo Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015 – 2016, amekuwa akifanya mazoezi ya peke yake tangu wiki iliyopita na sasa yuko tayari kurejea uwanjani.
  Pamoja na Abdul, majeruhi mwingine, kiungo chipukizi Baruan Akilimali naye ameanza mazoezi leo baada ya kupona, hivyo kufanya Juma Mahadhi awe majeruhi pekee aliyebaki kwenye kikosi cha Yanga SC.

  Juma Abdul (kushoto) akitafuta maarifa ya kumpita mchezaji wa Mbeya City msimu uliopita

  Yanga SC inatarajiwa kuteremka uwanjani Jumapili Saa 1:00 usiku kumenyana na Mbao FC katika mfululizo wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Na leo Ofisa Habari wa klabu, Dissmas Ten ametangaza viingilio vya mchezo huo ambavyo vitakuwa Sh. 15, 000 kwa VIP A, 10,000 VIP B na C na Sh. 5,000 kwa majukwaa mengine yaliyobaki ya mzunguko.  
  Kwa ujumla Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea Ijumaa kwa mchezo mmoja kati ya wenyeji, Lipuli ya Iringa dhidi ya Stand United Uwanja wa Samora.

  MECHI ZIJAZO LIGI KUU;
  Oktoba 5, 2018
  Lipuli v Stand United
  Oktoba 6, 2018
  Singida United v Ndanda FC
  Simba SC v African Lyon
  Kagera Sugar v Ruvu Shooting
  Tanzania Prisons v Mbeya City
  Mtibwa Sugar v KMC
  Oktoba 7, 2018
  Yanga SC v Mbao FC
  JKT Tanzania v Alliance FC
  Biashara v Nwadui FC
  Oktoba 8, 2018
  Azam v Coastal Union 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUMA ABDUL, AKILIMALI WAREJEA KUIONGEZEA NGUVU YANGA MECHI NA MBAO FC JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top