• HABARI MPYA

  Thursday, October 11, 2018

  GWIJI WA SOKA AFRIKA, SAMUEL ETO’O AZINDUA UJENZI WA UWANJA MPYA WA SOKA COCO BEACH LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  GWIJI wa soka Afrika, Samuel Eto’o leo amezindua ujenzi wa Uwanja wa soka maeneo ya Coco Beach mjini Dar es Salaam leo kwa udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager.
  Eto’o, ambaye kwa sasa anamalizia soka yake katika klabu ya Qatar SC katika shughuli hiyo aliambatana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob, Menena wa Bia ya Castle Lager Mchini, Pamela Kikuli na Balozi wa Castle Lager Tanzania, Ivo Mapunda.
  Eto’o alikwenda kupiga mpira na kufunga katika goli dogo huku umati wa waliojitokeza ukishangilia na hiyo ikawa maana yake ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira wa miguu maeneo ya Coco Beach umezunduliwa.
  Samuel Eto’o akipiga mpira kuzindua ujenzi wa Uwanja wa soka Coco Beach mjini Dar es Salaam leo 

  Samuel Eto'o (kulia) akiwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob (kusshoto) na Menena wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli 

  Mapema leo asubuhi, Eto’o mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Leganes, Espanyol, Mallorca, Barcelona zote za Hispania, Inter Milan ya Italia, Anzhi Makhachkala ya Urusi, Chelsea, Everton za England, Sampdoria ya Italia, Antalyaspor na Konyaspor za Uturuki aliendesha mafunzo ya soka kwa vijana wadogo katika hoteli ya Ramada, eneo la Kunduchi alipofikia.
  Mwanasoka huyo Bora Afrika mara nne katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010 aliwasili nchini jana jioni na anatarajiwa kuondoka kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA SOKA AFRIKA, SAMUEL ETO’O AZINDUA UJENZI WA UWANJA MPYA WA SOKA COCO BEACH LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top