• HABARI MPYA

  Saturday, October 06, 2018

  FIFA YAISIMAMISHA SIERRA LEONE BAADA YA SERIKALI KUINGILIA FA

  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeisimamisha uanachama Sierra Leone kufuatia Serikali ya nchi hiyo kuingilia shughuli za uendeshaji wa Chama cha Soka.
  Kifungo hicho kinakuja baada ya Tume ya Kuzuia Rushwa kumuondoa madarakani Rais wa SLFA, Isha Johansen na Katibu Mkuu wake, Christopher Kamara.
  "Kifungo hicho kitaondolewa iwapo tu SLFA na uongozi wake halali utaithibitishia FIFA kwamba viongozi walioondolewa wamerejeshwa ofisini," imesema FIFA.
  Iwapo kifungo hicho hakitaondolewa kabla ya Oktoba 11, mechi ya Sierra Leone dhidi ya Ghana kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 itafutwa pia - pamoja na ule wa marudiano na Black Stars Oktoba 15 nao upo hatarini.

  Sierra Leone ni miongoni mwa timu nne zenye pointi tatu katika Kundi F, ambalo linahusisha pia timu za Ethiopia na Kenya.
  Tume ya Kuzuia Rushwa (ACC) imesema chini ya sheria Sierra Leone, wote Johansen na Christopher Kamara lazima waachie nafasi zao hadi hapo kesi yao ya rushwa itakapokamilika.
  Wote Johansen na Kamara wamekanusha kufanya uovu wowote.
  FIFA imerudia kuionya Mamlaka ya Sierra Leone kwamba uamuzi wa ACC unaweza kugeuka kidungo, katika barua ya FIFA iliyosainiwa ya Katibu Mkuu wake, Fatma Samoura Septemba 28, imeitaka Serikali kumaliza tatizo hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAISIMAMISHA SIERRA LEONE BAADA YA SERIKALI KUINGILIA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top