• HABARI MPYA

  Monday, October 08, 2018

  ERASTO NYONI ATIWA HATIANI KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA NDANDA FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI mkongwe wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni atapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko Hassan Nassoro Maulid wa Ndanda SC katika mechi namba 33 iliyomalizika kwa sare ya 0-0 Septemba 15 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 

  Erasto Nyoni (kushoto) akisalimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli 

  Wambura amesema tukio la Nyoni, mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, halikuonwa na Mwamuzi wa mechi hiyo ndiyo maana hakuonyeshwa kadi.
  Aidha, Wambura amesema Simba wamepewa Onyo Kali kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake katika kikao cha maandalizi ya mechi hiyo na adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. 
  Wambura pia amesema kwamba Simba imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuwarushia chupa za maji na soda viongozi, wachezaji na kocha wao Mkuu, Mbelgiji Patrick J. Aussems baada ya mechi namba 48 dhidi ya Mbao FC walioshinda 1-0 Septemba 20 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kumalizika. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ERASTO NYONI ATIWA HATIANI KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA NDANDA FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top