• HABARI MPYA

  Tuesday, October 09, 2018

  DILUNGA AANZA MAZOEZI SIMBA SC LEO BAADA YA KUKOSEKANA KWA WIKI TATU AKIUGUZA KIFUNDO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Hassan Dilunga hatimaye leo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba SC baada ya kukosekana kwa takriban wiki tatu akisumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
  Dilunga aliumia Hassan Dilunga aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya Septemba 8, mwaka huu SImba SC ikishinda 4-2 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  Kiungo huyo mtaalamu alitolewa nje anachechemea dakika ya 57 nafasi yake ikichukuliwa na Said Ndemla na tangu hapo hajacheza tena.

  Hassan Dilunga akiwa mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba SC leo Uwanja Veterani mjini Dar es Salaam

  Na baada ya kukosekana kwa kipindi chote akijiuguza, hatimaye leo Dilunga ameibuka mazoezini Simba SC Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam.
  Kupona kwa kiungo huyo ni habari njema kwa Simba SC ambayo inapigana kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika msimu ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.
  Dilunga yupo katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe Simba SC kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro Julai mwaka huu alikodumu kwa msimu mmoja tu akitokea JKT Ruvu ya Dar es Salaam pia baada ya awali kuzitumimia Yanga SC na Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DILUNGA AANZA MAZOEZI SIMBA SC LEO BAADA YA KUKOSEKANA KWA WIKI TATU AKIUGUZA KIFUNDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top