• HABARI MPYA

  Monday, October 08, 2018

  BODI YAZIONYA VIKALI ASHANTI, KILUVYA UNITED NA MASHUJAA KWA MAKOSA DARAJA LA KWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), maarufu kama Kamati ya Saa 72 imezionya klabu za Daraja la Kwanza, Ashanti United ya Dar es Salaam, Kiluvya United ya Pwani na Mashujaa ya Kigoma kwa makosa mbalimbali.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
  Wambura amesema kwamba Ashanti United na Kiluvya United zote zimepewa Onyo Kali kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake katika kikao cha maandalizi ya mechi hiyo namba moja iliyomalizika kwa sare ya 1-1 Septemba 29 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
  Wambura Mgoyo amesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Na Mashujaa imeonywa kwa kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika tisa katika mechi namba mbili dhidi ya Polisi Tanzania walioshinda 2-0 Septemba 29 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma na  adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BODI YAZIONYA VIKALI ASHANTI, KILUVYA UNITED NA MASHUJAA KWA MAKOSA DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top