• HABARI MPYA

  Sunday, September 09, 2018

  ZIDANE KUINGIA NA WANNE MAN UNITED WAMO KROOS NA CAVANI

  MFARANSA Zinedine Zidane ameandaa orodha ya wachezaji wa kusajili kwenda kuiongezea nguvu Manchester United iwapo atakwenda kuchukua nafasi ya Mreno, Jose Mourinho anayetabiriwa kufukuzwa.
  Mourinho amejikuta katika wakati mgumu Old Trafford kufuatia mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya England akifungwa mechi mbili katika ya nne alizocheza.
  Mashetani Wekundu walipunguza kumpiga presha kocha huyo baada ya ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Burnley Uwanja wa Turf Moor wiki iliyopita, lakini Zidane ameendelea kuhusishwa na nafasi hiyo.
  Na kwa mujibu wa The Mirror, Mfaransa huyo tayari ameanza kuandaa mazingira yake atakapoingia kazini kwa kuandaa orodha ya wachezaji wa kusajili kwenda kuiongezea nguvu timu.

  Zinedine Zidane ameanza kuiunda upya Manchester United kuelekea kuchukua nafasi ya Jose Mourinho 

  Wachezaji anaowahitaji ni pamoja na Toni Kroos wa Real Madrid, Thiago Alcantara wa Bayern Munich, James Rodriguez – ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Bayern kutoka Real Madrid – na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani.
  Zidane alihitimisha maisha yake ya kazi Real Madrid siku chache tu baada ya kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi dhidi ya Liverpool mjini Kiev na tangu hapo hajafanya kazi.
  Wakati wake akiwa Bernabeu, Zidane pia alifanikiwa kutwaa taji la La Liga mwaka 2017 wakati pia alishinda taji la UEFA Super Cup na Klabu Bingwa ya Dumia ya FIFA kila moja mara mbili.
  Mourinho anatarajiwa kuingia katika kipindi cha kuamua hatima yake Manchester United baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya England kupisha mechi za kimataifa wikiendi hii. 
  United pia inatarajiwa kuanza mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa wamepangwa kundi moja na Young Boys na Valencia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE KUINGIA NA WANNE MAN UNITED WAMO KROOS NA CAVANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top