• HABARI MPYA

  Monday, September 10, 2018

  ZIDANE ASEMA MUDA SI MREFU ATAREJEA KUENDELEA NA KAZI

  KOCHA Zinedine Zidane amedokeza yuko karibuni kurejea kazini. Kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa amekuwa hana kazi tangu ajiuzulu ukocha wa Real Madrid baada ya kuwaongoza Los Blancos to kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Mei.
  Lakini ameliambia Shirika la Utangazaji la Kispaniola, TVE kwamba amepanga kurejea uwanjani muda mfupi sana. Zidane amesema; “Ndiyo, kweli. Hivi karibuni nitarejea mazoezini kwa sababu ni kitu ninachokipenda na ambacho nimekuwa nikikifanya maisha yangu yote,”.'
  Zidane anapewa nafasi kubwa ya kumbadili Jose Mourinho, iwapo Mreno huyo atafukuzwa Manchester United.

  Kocha Mfaransa, Zinedine Zidane amedokeza kwamba yuko karibuni kurejea kazini 

  Aliwaambia rafiki zake mwezi uliopita kwamba anatarajia kupewa ofa Old Trafford iwapo Mourinho ataondolewa. 
  Mourinho yuko hatarini kuondolewa baada ya mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya England msimu huu — United ikipoteza mechi mbili kati ya nne za awali.
  Na taarifa ya hivi karibuni kwenye gazeti la The Mirror imesema kwamba Zidane amekwishaanza kujiandaa kwa maisha mapya Old Trafford kwa kutayarisha orodha ya wachezaji wa kuingia nao. 
  Toni Kroos, Thiago Alcantara, James Rodriguez na Edinson Cavani wanatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliomo kwenye orodha ya Zidane ambao angependa kuingia nao Manchester akiteuliwa kumrithi Mourinho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE ASEMA MUDA SI MREFU ATAREJEA KUENDELEA NA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top