• HABARI MPYA

  Wednesday, September 05, 2018

  VAR KUFANYIWA MAJARIBIO LIGI KUU ENGLAND WIKI IJAYO

  SHERIA ya msaada wa Teknolojia ya Video (VAR) itafanyiwa majaribio katika Ligi Kuu ya England kwenye mechi 15 baada ya mapumziko ya sasa ya kupisha mechi za kimataifa.
  Sheria hiyo ya msaada wa video kwa marefa haikutumika kwenye Ligi Kuu ya England mwanzoni mwa msimu licha ya mafanikio yake katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.
  Lakini ligi hiyo kubwa sasa inataka kuichukua sheria hiyo katika mechi zote kuanzia msimu ujao.
  Na kutakuwa na majaribio ya mfumo huo ambayo yatafanyika kwenye mechi zaidi ya tano za Jumamosi Saa 9:00 jioni Septemba 15.

  Mechi hizo ni zitakazozihusisha Arsenal, Chelsea na Manchester City ambazo zitatazamwa na Maofisa wa video huko Stockley Park.
  Lakini uamuzi utakaochukuliwa kwenye video hautatumika uwanjani na hakutakuwa na mawasiliano baina ya marefa wanaochezesha mechi na Maofisa wa VAR.
  Lengo la ni kuona kama Maofisa wa video wanaweza kumudu kufanya zoezi hilo kwenye mechi nyingi kwa wakati mmoja.
  Ligi Kuu ya England ni kati ya ligi ambazo hazikuipokea sheria ya VAR haraka miongoni mwa ligi kubwa Ulaya.
  Sheria hiyo imekuwa ikitumika kwenye ligi zote, Bundesliga na Serie A tangu msimu uliopita, wakati La Liga imeanza kuitumia msimu huu.
  Teknologia hiyo ilitumika kwenye Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup msimu uliopita na itatumika zaidi msimu huu. VAR pia ilitumika kwenye fainali ya Kombe la FA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VAR KUFANYIWA MAJARIBIO LIGI KUU ENGLAND WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top