• HABARI MPYA

  Monday, September 17, 2018

  UCHAGUZI MDOGO KUZIBA NAFASI YA SANGA BODI YA LIGI KUFANYIKA NOVEMBA 17 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UCHAGUZI mdogo wa Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kujaza nafasi zilizo wazi utafanyika Jumamosi Novemba 17, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba Fomu kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa Septemba 21, mwaka huu kwenye ofisi za shirikisho hilo.
  "Muda wa mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni Saa 10:00 jioni Septemba 25, 2018,"amesema Ndimbo.
  Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Kuu (PL)L, Mjumbe mmoja kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL)FDL na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL).

  Clement Sanga alipoteza sifa za uongozi wa Bodi ya Ligi baada ya kujiuzulu uongozi wa Yanga SC 

  Ada ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti ni Sh. 200,000 (Shilingi laki mbili)mbili wakati nafasi nyingine zilizobaki ni sh.100,000 (Shilingi laki moja).
  Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
  Wagombea kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ni marais au Wenyeviti wa Klabu husika, Hivyo, Wagombea wanatakiwa kuwa Wenyeviti au Marais wa Klabu husika. 
  Nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB inagombewa na Klabu za Ligi Kuu pekee. Ikumbukwe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Clement Sanga alipoteza sifa baada ya kujiuzulu uongozi wa klabu yake, Yanga SC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI MDOGO KUZIBA NAFASI YA SANGA BODI YA LIGI KUFANYIKA NOVEMBA 17 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top