• HABARI MPYA

    Friday, September 14, 2018

    TFF YABADILI MFUMO WA MICHUANO YA KOMBE LA AZAM SPORTS, SASA KUANZIA NGAZI YA WILAYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSIMU mpya wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation (ASFC) inatarajiwa kuanza mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
    Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi alipozungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dar es Salaam.
    Madadi amesema kwamba tofauti na misimu iliyotangulia, safari hii mashindano hayo yatakuwa na mfumo mpya, kwani yataanzia katika ngazi ya wilaya. 

    “Tumeelekeza mashindano haya sasa yaanze kwenye ngazi ya Wilaya, tumewapa majukumu vyama vya mpira vya mikoa, kuhakikisha wilaya zinacheza kupata bingwa, na mikoa inacheza kumpata bingwa, kwa hiyo akipatikana bingwa wa mkoa, na mabingwa wa ligi ya mikoa, wale wataanza pale kwenye awamu ya mwanzo, awamu ya awali kushindana, kabla ya hatua ambazo zitaingiza timu za Daraja la Pili, la Kwanza na baadaye Ligi Kuu,”amesema Madadi.
    Aidha, kocha huyo wa zamani wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, amesema mashindano ya mwaka huu yatakuwa ni bora zaidi na yatakuwa na ushindani mkubwa kuliko msimu uliopita. 
    Mtibwa Sugar ndio mabingwa watetezi wa ASFC baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United kwenye fainali Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
    Na walikuwa mabingwa watatu tangu michuano hiyo irejeshwe mwaka 2016, baada ya Yanga SC na Simba SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YABADILI MFUMO WA MICHUANO YA KOMBE LA AZAM SPORTS, SASA KUANZIA NGAZI YA WILAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top