• HABARI MPYA

  Wednesday, September 05, 2018

  TANZANIA YAFUZU BILA JASHO FAINALI ZA SOKA YA UFUKWENI BAADA YA AFRIKA KUSINI KUJITOA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya taifa ya soka la ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Misri, kufuatia waliokuwa wapinzani wao kwenye mechi ya mchujo, Afrika Kusini kujitoa. 
  Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba timu ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali hizo baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano. 
  Ndimbo amesema Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limewajulisha TFF juu ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.

  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9,2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAFUZU BILA JASHO FAINALI ZA SOKA YA UFUKWENI BAADA YA AFRIKA KUSINI KUJITOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top