• HABARI MPYA

    Saturday, September 15, 2018

    TAKUKURU YAWATAKA HANS POPPE NA LAUWO KUJISALIMISHA WAJUMUISHWE KWENYE KESI YA AKINA AVEVA NA KABURU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Julius Mbungo amewataka mfanyabiashara Zacharia Hans Poppe na Mhandisi Frank Lauwo ambao kujisalimisha baada ya kutafutwa kwa muda mrefu.
    Wawili hao wanatakiwa ili kujumuishwa katika katika kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa klabu ya Simba SC, aliyekuwa Rais, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu au kuifuta kesi hiyo.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana mjini Dar es Salaam, Brigedia Jenerali Mbungo amesema atakayesaidia kupatikana kwa wawili hao atapatiwa zawadi.
    Jenerali Mbungo alisema kwamba Hans Poppe yeye alitoa taarifa za uongo kwenye Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwamba Simba SC walinunua nyasi za bandia kutoka kampuni moja ya China kwa thamani ya dola za Kimarekani 40,0577 wakati si kweli. 


    “Lakini uhalisia kamili ni kwamba, zile nyasi zilinunuliwa kwa dola 109,499. Nia hapa ilikuwa ni kutolipwa mapato yanayotakiwa kulipwa TRA, Franklin Peter Lauwo yeye huyu bwana alipata huu ukandarasi kwa njia ya rushwa, kwa sababu alikuwa hana sifa, alikuwa si mkandarasi aliyesajiliwa,”alisema Jenerali Mbungo. 
    Kutopatikana kwa wawili hao ambao walitafutwa hadi kwa msaada wa Interpol kwa muda mrefu kulisababisha kesi hiyo kuchelewa hadi washitakiwa wote wakamilike.
    Na Agosti 10, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa hao wawili katika kesi hiyo.
    Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema bado wanaifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu lakini itafika mahali uvumilivu utawashinda na kama Jamhuri wameshindwa basi waifute.
    Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.
    Wanadaiwa, kuwa  Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAKUKURU YAWATAKA HANS POPPE NA LAUWO KUJISALIMISHA WAJUMUISHWE KWENYE KESI YA AKINA AVEVA NA KABURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top