• HABARI MPYA

  Wednesday, September 05, 2018

  TAIFA STARS KUONDOKA KESHO MCHANA KUIFUATA UGANDA MECHI JUMAMOSI JIONI NAMBOOLE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuondoka kesho Saa 7:00 mchana kwenda mjini Kampala kwa ajili ya mchezo na wenyeji, Uganda Jumamosi Uwanja wa Mandela, Namboole kutafuta tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani ncini Cameroon.
  Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba Taifa Stars itaondoka na kikosi cha wachezaji 23 na viongozi saba, wakiwemo wa shirikisho hilo.
  “Ni mchezo tunaokwenda kwa nia ya kufanya vizuri na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kundi letu. Kufanya vizuri kwa timu hii ni fahari ya kila Mtanzania tuendelee kuiunga mkono timu hii inayokwenda kupeperusha bendera ya Tanzania,” amesema Ndimbo.
   
  Kwa upande wake, Kocha Emmanuel Amunike anasema anaendelea na maandalizi akiendelea kuangalia mapungufu mbalimbali na kuyafanyia kazi ambapo anaamini kikosi kilichopo huku wachezaji wanaocheza nje wakiwa wameripoti wote.  
  Amunike aliyesaini mkataba wa kufundisha Taifa Stars mapema Agosti akichukua nafasi ya mzalendo, Salum Mayanga amesema kikosi kina muelekeo mzuri na maelekezo anayotoa anaona yanaeleweka. 
  Naye Nahodha Mbwana Samatta amesema mchezo huo utakuwa wa ushindani na kikubwa ni kufuata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.
  Wachezaji wanaotarajiwa kusafiri ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Benno Kakolanya (Yanga SC), Mohammed Abdulrahman Wawesha (JKU).
  Mabeki; Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), David Mwantika (Azam FC), Ally Sonso (Lipuli FC), Paul Ngalema (Lipuli FC), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam FC).
  Viungo; Himid Mao (Petrojet, Misri), Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Frank Domayo (Azam FC), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar), Mudathir Yahya (Azam FC), Farid Mussa (CD Tenerife, Hispania) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadida, Morocco).
  Washambuliaji; Yahya Zayed (Azam FC), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Shaaban Iddi Chilunda (CD Tenerife, Hispania), Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana), Thomas Ulimwengu (El HIlal Omduran, Sudan)  na Nahodha, Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).
  Amunike anasadiwa na Hemed Morocco na Mnigeriua mwenzake, Emeka Amadi, wakati Mtunza Vifaa ni Ally Ruvu na madaktari wawili Richard Yomba na Gilbert Kigadya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUONDOKA KESHO MCHANA KUIFUATA UGANDA MECHI JUMAMOSI JIONI NAMBOOLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top