• HABARI MPYA

    Tuesday, September 11, 2018

    SHABIKI WA SIMBA ANAYESOMA CHUO KIKUU CHA IRINGA AJISHINDIA SH. MILIONI 239.4 ZA M-BET

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.
    Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za ulaya.
    Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect 12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.
    Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu.






    Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. 
    Sh Milioni 239.4 

    “Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10 ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.
    Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo.
    Akizungumza  baada ya kupokea hundi yake, Mbwilo alisema kuwa amefarijika sana kupata fedha hizo ambazo atazitumia kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo, kuwasomesha ndugu zake na kusaidia familia.
    Mbwilo alisema kuwa pia atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya kuuza matofali na kuanzisha biashara nyingine.
    Alisema kuwa yeye ni mtoto yatima na aliishi maisha ya mitaani huku akiokota taka na kuziuza kama mbolea (samadi) kwa akina mama ambao walikuwa wateja wake kwa lengo la kumsaidia.
     “Niliishi mitaani, nilikwenda jalalani kutafuta matunda, taka, kutafuta taka na kuziuka kama mbolea, nilifanya hivyo baada ya kuachwa na mlezi wangu nikiwa kidato cha pili, naguswa na aina hiyo ya watoto yatima hiyo.
    “Tarehe 6 mwezi huu, nilitumia sh 1,000 kubashiri na kupata kiasi kikubwa cha fedha, namshukuru Mungu kwani wanaobashiri wengi, nitasaidia kituo cha watoto yatima kwa kunua magodoro, kuna kituo cha watoto yatima ambao hawana vitanda hata magodoro, nitafanya hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nimetokea huko,” alisema Mbwilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHABIKI WA SIMBA ANAYESOMA CHUO KIKUU CHA IRINGA AJISHINDIA SH. MILIONI 239.4 ZA M-BET Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top