• HABARI MPYA

  Tuesday, September 04, 2018

  RONALDO ANALIPWA MARA TATU ZAIDI YA ANAYEMFUATIA SERIE A

  NYOTA wa Juventus, Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Serie A na anaingiza mara tatu zaidi ya mchezaji anayemfuatia kwa kulipwa kwenye ligi hiyo.
  Hata hivyo, Ronaldo hadi sasa hajadhihirisha thamani ya malipo hayo makubwa, akiwa amecheza mechi tatu bila kuwafungia bao mabingwa wa Serie A tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 100 kutoka Real Madrid msimu huu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amejikuta anaongeza kipato chake baada ya kuhama mji mkuu wa Hispania, Madrid na kutua Italia ambako sasa analipwa mshahara wa Pauni Milioni 28 kwa mwaka.
  Ni Lionel Messi anayelipwa Pauni Milioni 40.5 kwa mwaka Barcelona na Neymar Pauni Milioni 31.7 Paris Saint-Germain pekee wanaopokea mishahara mikubwa kuliko Ronaldo. 
  Kwa mujibu wa taarifa katika gazeti la Gazzetta dello Sport, Ronaldo anapata mshahara wa Pauni 538,000 kila wiki. 
  Mishahara ya wachezaji wengine wenye majina makubwa wanaocheza Italia ni midogo mno ukilinganisha na wa Ronaldo, huku Gonzalo Higuain akiw anayemfuatia kama mchezaji wa pili kwa kulipwa zaidi kwenye ligi hiyo.
  Mshambuliaji huyo Muargentina bado anapokea Pauni Milioni 8.5 kwa mwaka kutokana Pauni 165,000 anazopata kwa wiki, baada ya kodi kufuatia kuhamia AC Milan akitokea Juventus.
  Katika wachezaji 11 wanaolipwa zaidi kwenye ligi hiyo ukiondoa Gianluigi Donnarumma wa AC Milan Pauni Milioni 5.4 kwa mwaka), Lorenzo Insigne wa Napoli Pauni Milioni 4.1 kwa mwaka, Mauro Icardi wa Inter Milan Pauni Milioni 4 kwa mwaka na Edin Dzeko wa AS Roma Pauni Milioni 4 kwa mwaka, wengine wote ni wa Juve. 

  Cristiano Ronaldo analipwa mara tatu zaidi ya mchezaji anayemfuatia kwa kulipwa Serie A 

  ORODHA YA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI SERIE A 

  1. Cristiano Ronaldo (Juventus) - £31m 

  2. Gonzalo Higuain (AC Milan) - £8.5m

  3. Paulo Dybala (Juventus) - £6.3m 

  4. Miralem Pjanic (Juventus) - £5.8m

  5. Douglas Costa (Juventus) - £5.4m

   6. Ginaluigi Donnarumma (AC Milan) - £5.4m

  7. Leonardo Bonucci (Juventus) - £5m

  8. Emre Can (Juventus) - £4.5m

  9. Lorenzo Insigne (Napoli) - £4.1m

  10. Mauro Icardi (Inter Milan) - £4m

  11.  Edin Dzeko (Roma) - £4m

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO ANALIPWA MARA TATU ZAIDI YA ANAYEMFUATIA SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top