• HABARI MPYA

  Monday, September 17, 2018

  RAYON YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA ENYIMBA NYAMIRAMBO

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  WENYEJI, Rayon Sports jana wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Enyimba ya Nigeria katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
  Sare hiyo inawapa mzigo wapendwa hao wa Rwanda wa kuelekea mchezo wa marudiano Jumapili ya Septemba 23 Uwanja wa Enyimba International mjini Aba, ambako watatakiwa kwenda kushinda, ama kutoa sare ya mabao, au wakitoa sare ya 0-0 tena washinde kwa mikwaju ya penalti ili kwenda Nusu Fainali.
  Mechi nyingine za Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho jana, bao pekee la  Mahmoud Wadi dakika ya 54 lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Al Masry dhidi ya USM Alger ya Algeria Uwanja wa Port Said mjini Cairo, Misri.

  Mshambuliaji Jean-Marc Makusu akafunga mabao mawili dakika za 44 na 57 kabla ya kumsetia beki Juma Shabani kufunga la tatu dakika ya 78, AS Vita ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya RSB Berkane ya Morocco ambayo bao lake la ugenini lilifungwa na Mohammed Aziz dakika ya 24 Uwanja wa Martyrs de la Pentecote mjini Kinshasa, DRC.
  Raja Cassablanca wakapata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, CARA Brazzaville Uwanja wa Alphonse Massamba-Débat mjini Brazzaville.
  Mabao ya Raja yalifungwa na Soufiane Rahimi dakika ya 47 na Mahmoud Benhalib dakika ya 80, wakati la CARA lilifungwa na Cabwey Mereves Kivutuka dakika ya 71.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAYON YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA ENYIMBA NYAMIRAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top