• HABARI MPYA

  Monday, September 03, 2018

  NI RAYON NA ENYIMBA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, USM ALGER NA EL MASRY

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  TIMU ya Rayon Sport ya Rwanda itamenyana na Enyimba ya Nigeria katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwezi ujao.
  Hiyo ni baada ya droo ya Robo Fainali ya michuano hiyo iliyopangwa leo mjini Cairo nchini Misri, yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika,
  Na Rayon Sport wataanzia nyumbani Oktoba 16 kabla ya kusafiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano Oktoba 23.

  Rayon Sport itamenyana na Enyimba katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwezi ujao

  USM Alger iliyokuwa kundi moja na Rayon, pamoja na Yanga SC ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya imepangiwa jirani zao wa Kaskazini mwa Afrika, El Masry ya Misri na wataanzia ugenini. El Masry iliitoa Simba SC ya Tanzania katika Raundi ya pili ya mchujo Kombe la Shirikisho.

  CARA ya Kongo itamenyana na Raja Cassablanca ya Morocco, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na RS Berkane ya Morocco.
  Mechi zote za kwanza zitafanyika Oktoba 16 na za marudiano zitafanyika Oktoba 23, mwaka huu.
  Na katika Ligi ya Mabingwa;  Primiero de Agosto ya Angola itamenyana na TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Etoile du Sahel, ES Setif ya Algeria na Wydad Casablanca ya Morocco na Horoya ya Guinea dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
  Mechi za kwanza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitafanyika kati ya Septemba 14 na 15 na marudiano yatafuatia kati ya Septemba 21 na 22, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI RAYON NA ENYIMBA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, USM ALGER NA EL MASRY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top