• HABARI MPYA

  Monday, September 17, 2018

  NDEGE MAALUM KUIPELEKA TAIFA STARS HARAKA CAPE VERDE NA KURUDI DAR KWA MECHI ZA NYUMBANI NA UGENINI

  Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Sola Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini, kampuni ya Serengeti wanataka kuandaa ndege maalum ya kuipeleka timu ya taifa nchini Cape Verde na kuirudisha kwa ajili ya mechi mbili za nyumbani na ugenini za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani Cameroon.
  Cape Verde watakuwa wenyeji wa Tanzania Oktoba 12, mwaka huu Uwanja wa Taifa wa Cape Verde mjini Praia katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON 2019 mwakani nchini Cameroon, kabla ya timu hizo kurudiana Oktoba 16 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Na leo Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kwamba shirikisho hilo kwa kushirikiana na wadhamini wa Taifa Stars, SBL wanafanya utaratibu wa usafiri utakaoipeleka na kuirudisha timu ya Taifa kulingana na ratiba ya michezo hiyo ilivyokaa.
  “Utaratibu wa kambi, kikosi walimu watauzungumza ambao utazingatia umuhimu wa mchezo,tarehe za kuondoka na tarehe za michezo yote miwili. Unafanyika utaratibu wa kusafiri na mashabiki wa timu ya Taifa ambao watachangia gharama kidogo. Tumekuja na Hashtag itakayotumika katika safari yetu ya kutupeleka Cameroon kwenye fainali hizo za mwakani #AfconCameroon2019ZamuYetu,”imesema taarifa ya Ndimbo. 
  Ndimbo ametoa rai kwa Vyombo vya Habari nchini kuungana pamoja kwa kuwa ni sehemu muhimu katika safari hiyo ya kwenda Cameroon. “Wadau mbalimbali tuungane pamoja Tanzania ni yetu,Taifa Stars ni timu yetu,” amesema.
  Kwa sasa katika Kundi L Uganda ndiyo wanaoongoza kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho na Tanzania wenye pointi mbili kila mmoja baada ya kila timu kucheza  mechi mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDEGE MAALUM KUIPELEKA TAIFA STARS HARAKA CAPE VERDE NA KURUDI DAR KWA MECHI ZA NYUMBANI NA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top