• HABARI MPYA

  Monday, September 17, 2018

  MTIBWA SUGAR YAMUONGEZEA MKATABA KIUNGO WAKE SALEH KHAMIS ABDALLAH HADI 2021

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa  Azam Sports Federation Cup, Mtibwa Sugar wame endelea kuimarisha kikosi chao baada ya kufanikiwa kumuongezea  mkataba mpya na kiungo wake Saleh Khamis Abdallah (pichani kushoto).
  Abdallah  alikuwa anatumikia mwaka wake wa mwisho ambao ungemalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa ameongeza miaka miwili hivyo  ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021.
  Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa klabu, Abubakar Swabr amesema kwamba wameuboresha mkataba wa awali wa kiungo huyo na hivyo ataendelea kuitumikia Mtibwa hadi 2021.
  “Saleh ni mchezaji mzuri sana na ameitumikia klabu hii kwa kiwango cha hali ya juu kabisa na hivyo uongozi pamoja na Saleh tumekaa pamoja na  tumefikia makubaliano ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021 na hii ni baada ya kuongeza miaka 2, ni furaha kwetu kwa kwakuwa tumemuongeza mkataba mtu sahihi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho” Abubakar Swabr
  Saleh alikuzwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na baadae alienda kucheza soka la kulipwa Msumbiji kabla ya kurejea msimu wa 2016 katika usajili wa dirisha dogo kujiunga na Mtibwa Sugar tena kwa kandarasi ya miaka miwili na miezi sita ambayo ilikuwa inafika tamati mwisho wa msimu huu.
  Kiungo huyo mshambuliaji pia ametoa mchango mkubwa kwa wana tam tam msimu 2017/2018 baada kuwa mmoja ya wachezaji waliobeba Kombe la Azam Sports Federation Cup.
  Msimu huu Saleh tayari amecheza mchezo mmoja tu dhidi ya Simba katika ngao ya jamii na kufanikiwa kutoa pasi ya goli (assist) katika mchezo huo ambo tulipoteza kwa 2-1, baada ya hapo Saleh hajafanikiwa kucheza kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo huo na kwa mujibu wa report ya madaktari wa Mtibwa Sugar anatarajia kurejea mazoezini wiki hii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMUONGEZEA MKATABA KIUNGO WAKE SALEH KHAMIS ABDALLAH HADI 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top