• HABARI MPYA

  Thursday, September 13, 2018

  MTIBWA SUGAR YAMTIA KITANZI MCHEZAJI BORA KOMBE LA TFF, ISMAIL AIDAN MHESA HADI 2021

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa  Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mtibwa Sugar wamefanikiwa kuingia mkataba mpya na kiungo wake mshambuliaji Ismail Aidan Mhesa.
  Mhesa alikuwa anatumikia mwaka wake wa mwisho ambao ungemalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa ameongeza miaka miwili hivyo Ismail Aidani Mhesa ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021.
  Akizungumza na tovuti hii leo, Abubakar Swabr juu ya mkataba wa Mhesa amesema wameboresha mkataba wa awali na hivyo ataendelea kuitumikia Mtibwa hadi 2021.
  Ismail Aidan Mhesa ataendelea kuitumikia Mtibwa Sugar hadi mwaka 2021
  Ismail Aidan Mhesa akisaini mkataba mpya Mtibwa Sugar leo

  “Tumefikia makubaliano na Ismail Aidan Mhesa ya kuongeza miaka miwili na alikuwa anatumikia mwaka wake wa mwisho hivyo tumefikia makubaliano ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021, ni furaha kwetu kwa kwakuwa tumemuongeza mkataba mtu sahihi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho” amesema Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabr.
  Ismail Aidan Mhesa alijiunga na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar tangu 2014 na mwaka jana alipandishwa hadi kikosi cha timu ya wakubwa akitokea timu ya  vijana ya Mtibwa Sugar.
  Kiungo huyo mshambuliaji pia ametoa mchango mkubwa kwa wana tam tam msimu 2017/2018 baada kuwa mmoja ya wachezaji waliobeba kombe la Azam Sports Federation Cup.
  Huyo ni Mchezaji huyo Bora wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), Azam Sports Federation Cup (ASFC) katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Singida United Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Na msimu huu ameuanza vizuri baada ya kufunga bao moja katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMTIA KITANZI MCHEZAJI BORA KOMBE LA TFF, ISMAIL AIDAN MHESA HADI 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top