• HABARI MPYA

  Friday, September 07, 2018

  MTIBWA SUGAR LEO WANACHEZA NA MAWEZI MANUNGU NA JUMAPILI WATAKIPIGA NA AFC LEOPARDS CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar leo Saa 10:00 jioni itacheza mechi ya kirafiki na Mawenzi Market Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na baada ya hapo kesho asubuhi itapanda basi kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo na AFC Leopards ya Kenya Jumapili.
  Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba mchezo na Leooards, vigogo wa Kenya na Afrika Mashariki kwa ujuml utafanyika Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

  Kocha Zubery Katwila anataka kutumia michezo hiyo ya kirafiki kukiweka sawa kikosi chake wakati huu Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesimama kupisha mchezo wa kimataifa baina ya Tanzania na Uganda utakaofanyika kesho mjini Kampala.
  Mtibwa Sugar imeshinda mechi mbili kati ya tatu za awali za Ligi Kuu, 1-0 na Tanzania Prisons na 2-1 na Mbeya City zote Manungu, ikitoka kufungwa 2-1 na Yanga SC kwenye mechi ya kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na kocha Katwila, mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar anataka kuendeleza wimbi la ushindi Ligi Kuu itakaporejea wiki ijayo na ndiyo maana anakiweka sawa kikosi chake kwa mechi za kujipima ili kuona mabadiliko baada ya kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza kwenye mechi za awali. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR LEO WANACHEZA NA MAWEZI MANUNGU NA JUMAPILI WATAKIPIGA NA AFC LEOPARDS CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top