• HABARI MPYA

  Saturday, September 15, 2018

  MOURINHO: KAMA POGBA HAJANIAMBIA ANATAKA KUONDOKA, MAANA YAKE ANABAKI

  KOCHA Mreno, Jose Mourinho amekiri yuko kizani juu ya mustakabali wa kiungo Paul Pogba na amemtaka Mino Raiola kusema wazi mpango wake kwa kiungo huyo wa Manchester United.
  Pogba alizungumzia uhamisho wa kwenda Barcelona alipokuwa amekwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Ufaransa wiki iliyopita na aliwaambia wachezaji wenzake anataka kuondoka Old Trafford.
  Bosi huyo wa United amesema kwamba hana uhakika nini Raiola anatengeneza nyuma ya pazia juu la safari yake ya Watford leo.
  "Kama ninamuona Raiola kwenye kioo anasema wachezaji wanataka kuondoka, na hivyo ndiyo anaandaa njia ya yeye kujaribu kuondoka, kisha nitaamini," alisema Mourinho.
  "Kwa wakati huu, nipo kizani. kitu pekee kilichopo wazi kwangu ni kwamba mchezaji huyo hajawahi kabisa kunitamkia siku zote tunazokuwa pamoja kwamba anataka kuondoka. Pia ninataka wakala naye aniambie, au awaambie ukweli katika namna ambayo ninaweza kuona," amesema Mourinho.
  Raiola amekuwa na mazungumzo na Barcelona tangu mwishoni mwa msimu na wingu limetanda kwenye maisha ya Pogba United kufuatia mwanzo mbaya wa msimu.
  Mourinho alisema: "Kama hajaniambia anataka kuondoka, ni kwa sababu anataka kubaki. Hilo ndilo hitimisho langu," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO: KAMA POGBA HAJANIAMBIA ANATAKA KUONDOKA, MAANA YAKE ANABAKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top