• HABARI MPYA

  Sunday, September 09, 2018

  MHILU ATOKEA BENCHI KUCHUKUA NAFASI YA NGASSA NA KUIFUNGIA YANGA SC IKIILAZA 1-0 AFRICAN LYON

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la kiungo Yussuf Mhilu dakika za lala salama, limeipa ushindi mwembamba wa 1-0 Yanga SC dhidi ya African Lyon katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mhiliu alifunga bao hilo dakika ya 84 kwa kichwa akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa Kasebo Douglas wa Lyon kufuatia shuti la mshambuliaji Matheo Anthony kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
  Lakini wachezaji wa Lyon walinyoosha mikono kulalamika kwamba Matheo alipiga mpira ukiwa nje ya Uwanja, ingawa ulionekana upo kwenye chaki na mguu wa mpigani ndiyo ulikuwa nje.

  Yussuf Mhilu ametokea benchi na kuifungia Yanga bao pekee ikiilaza 1-0 African Lyon leo  PICHA YA MAKTABA

  Mtengenezaji wa nafasi na mfungaji wote walitokea benchi kipindi cha pili, Matheo akimbadili Pius Buswita na Mhilu akichukua nafasi ya mkongwe na Nahodha wa leo, Mrisho Ngassa.
  Mkongwe Haruna Moshi ‘Boban’ aliiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya Lyon na kumjaribu kipa wa Yanga, Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa mashuti kadhaa ambayo hayakuwa na madhara. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Klaus Kindoki, Paul Godfrey, Simon Gustavo/Jaffar Mohammed, Cleophas Sospeter, Said Juma ‘Makapu’, Raphael Daudi/Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita/Matheo Anthony, Deus Kaseke/Ibrahim Ajib, Heritier Makambo/Amissi Tambwe na Mrisho Ngassa/Yussuf Mhilu.
  African Lyon; Kasebo Douglas, Halfani Mbarouk, Kassim Simbaulanga, Augustino Samson, Daud Salum, Baraka Jaffar Awadh Salum/Kassim Kilungo, Ismail Adam, Victor Da Costa/Adam Omar, Haruna Moshi ‘Boban’ na Gervas Bernard.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MHILU ATOKEA BENCHI KUCHUKUA NAFASI YA NGASSA NA KUIFUNGIA YANGA SC IKIILAZA 1-0 AFRICAN LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top