• HABARI MPYA

  Monday, September 03, 2018

  MESSI NJE, FAINALI NI RONALDO, SALAH NA MODRIC

  MSHAMBULIAJI Muargentina, Lionel Messi hajaingia fainali ya tuzo za Mchezaji Bora wa Kiume wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), huku Cristiano Ronaldo, Mohamed Salah na Luka Modric wakiingia. 
  Mkali huyo wa Barcelona alifunga mabao 44 msimu uliopita na kuisaidia timu yake kutwaa mataji ya La Liga na Copa del Rey. 
  Yeye na timu yake, Argentina walitolewa katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia na Ufaransa walioibuka mabingwa na kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 11 hajafikiriwa miongoni mwa wanasoka bora wa dunia.
  Alikuwa mshindi wa pili mwaka 2007 na 2008 kabla ya kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2009 katika miaka mitano. 
  Ronaldo, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka jana, anatarajiwa kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji walioingia fainali, lakini bado anapewa nafasi kubwa ya kushinda. 
  Salah amekuwa tegemeo la Liverpool, akifunga mabao 43 kwenye mashindano yote msimu uliopita na kukisaidia kikosi cha Jurgen Kloop kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa, ambako alilazimika kuondoka uwanjani baada ya kuumia bega. Alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya England na ni mshindani mkuu.
  Real Madrid walifanikiwa kutetea taji lao katika fainali ya Ulaya, na pamoja na ukweli kwamba hakufunga, lakini Ronaldo akainua taji hilo kwa mara ya tano katika historia yake.
  Baada ya hapo, Mreno huyo akahamia Juventus kwa ada ya Pauni Milioni 100 na atashindana na mchezaji mwenzake wa zamani, Modric katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Msimu.
  Mcroatia huyo aliisaidia timu yake ya taifa kufika fainali ya Kombe la Dunia na alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Real Madrid cha kocha  Zinedine Zidane. 
  Kwa upande wake, Zidane naye anawania tuzo hiyo katika kipengele cha Kocha Bora, akishindanishwa na kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps na wa Croatia, Zlatko Dalic  alioingia fainali. 
  Washindi watatangazwa Septemba 24 Jijini London baada ya kukamilika kwa zoezi la kupiga kura litakalohusisha makocha, waandishi wa Habari na mashabiki.


  ORODHA KAMILI YA WANAOWANI TUZO ZA FIFA: 

  Mchezaji Bora wa Kiume - Cristiano Ronaldo, Luka Modric, Mo Salah
  Mchezaji Bora wa Kike - Ada Hegeberg, Dzsenifer Maroszan, Marta
  Tuzo ya Shabiki wa FIFA - Sebastian Carrera, Japan and Senegal supporters, Peru Supporters
  Kocha Bora wa Kike - Reynald Pedros, Asako Takakura, Sarina Wiegman
  Kocha Bora wa Kiume - Zlatko Dalic, Zinedine Zidane, Didier Deschamps
  Tuzo ya Puskas - Gareth Bale, Denis Cheryshev, Lazaros Christodoulopoulos, Cristiano Ronaldo, Giorgian De Arrascaeta, Riley McGree, Lionel Messi, Benjamin Pavard, Ricardo Quaresma, Mo Salah 
  Kipa Bora -  Thibaut Courtois, Hugo Lloris, Kasper Schmeichel
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI NJE, FAINALI NI RONALDO, SALAH NA MODRIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top