• HABARI MPYA

  Monday, September 10, 2018

  ‘MAPRO’ WA SIMBA SC KUANZA KUREJEA KESHO, MECHI IJAYO JUMAMOSI NA NDANDA FC NANGWANDA SIJAONA

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa Simba SC waliokuwa na timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa mwishoni mwa wiki wanatarajiwa kuanza kurejea kesho kuungana na wenzao kwa maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu.
  Kocha Mtunisia wa mazoezi ya viungo wa Simba SC, Adel Zrane amesema kwamba, wachezaji waliokuwa Uganda beki Juuko Murshid na mshambuliaji Emmanuel Okwi watarudi kesho.
  Lakini kuhusu kiungo Mzambia, Cletus Chama Mtunisia huyo amesema anaweza kurudi kesho kutwa ingawa akashindwa kutaja siku ya kurejea kwa kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Meddie Kagere kutoka Rwanda.

  Kiungo Mzambia, Cletus Chama (kushoto) anatarajiwa kurejea keshokutwa

  “Okwi na Kagere wanarudi kesho, Chama hatoweza kurudi kesho labda kesho kutwa hivyo. Tunategemea hivi karibuni tutakua na kikosi chetu kamili na kama mnavyoona kipa wetu Aish Manula naye amerejea kutoka timu ya taifa ya hapa na leo tulikuwa naye katika mazoezi,” alisema.
  Baada ya mwanzo mzuri katika Ligi Kuu wakishinda mechi mbili mfululizo dhidi ya timu za Mbeya, 1-0 na Tanzania Prisons na 2-0 na Mbeya City, zote Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Simba SC wanatarajiwa kusafiri kwa mara ya kwanza kwa mchezo wa ugenini.
  Kikosi hicho cha kocha Mbelgiji, Patrick J Aussems kitakuwa ugenini kwa Ndanda FC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwa mchezo wa tatu wa msimu.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘MAPRO’ WA SIMBA SC KUANZA KUREJEA KESHO, MECHI IJAYO JUMAMOSI NA NDANDA FC NANGWANDA SIJAONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top