• HABARI MPYA

  Wednesday, September 05, 2018

  MANYIKA ASEMA SINGIDA UNITED WAMEMVUNJIA MKATABA, DIRISHA DOGO ANAHAMIA TIMU NYINGINE

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KIPA Peter Manyika amesema kwamba Singida United imevunja mkataba naye baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu, hivyo amejiondoa rasmi na sasa ni mcheza huru.
  Akizungumza mjini Dar es  Salaam leo, Manyika amesema kwamba baada ya kushindwa kumpa stahiki zake nyingine za kimkataba, Singida United imeshindwa pia na kumlipa mishahara.
  Amesema kwamba sababu hiyo amejiondoa kwenye timu anasubiri dirisha dogo aende kusaini timu nyingine aendelee na kazi.

  Peter Manyika amesema amejiondoa rasmi Singida United baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu 

  “Wamenirudisha nyuma sana, mwanzo niliwaomba wanipe barua mapema ya kuniruhusu kuondoka, wao wakasema watalipa kila kitu nachodai kabla msimu haujaanza. Hadi sasa hivi hawajafanya chochote na wapo kimya,”
  “Hivyo mkataba unasema kama hutaweza kumlipa mchezaji mishahara kwa miezi mitatu utakua umeuvunja. Hiyo miezi mitatu ilikwishapita, hilo ni moja kati ya mengi waliyoshindwa, hivyo dirisha dogo naweza kwenda popote ili nimalizie ligi,”amesema Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Manyika Peter aliyewika klabu ya Yanga.  
  Kwa sasa Manyika anafanya mazoezi kwenye kituo kinachosimamiwa na baba yake, Manyika ambaye pia ni kocha wa makipa wa timu za vijana za taifa.
  Manyika mdogo alikuwa anauanza msimu wa pili Singida United baada ya kujiunga nayo kutoka Simba SC, klabu yake ya kwanza kabisa kwenye soka ya ushindani baada ya kuibukia shule na kuchaguliwa hadi timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANYIKA ASEMA SINGIDA UNITED WAMEMVUNJIA MKATABA, DIRISHA DOGO ANAHAMIA TIMU NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top