• HABARI MPYA

  Sunday, September 09, 2018

  SHAW: NINAENDELEA VIZURI NA NIPO KWEYE MIKONO SALAMA

  BEKI wa England, Luke Shaw amesema anaendelea vizuri na anatarajia atarejea uwanjani mapema baada ya kuumia jana katika mchezo dhidi ya Hispania nyumbani.
  Shaw ametweet: "Asanteni wote kwa upendo na sapoti yenu. Ninaendelea vizuri na nipo kwenye mikono salama. Mimi ni mpiganaji, hivyo nitarejea hivi karibuni!,"' 
  Kocha wa England, Gareth Southgate amethibitisha Luke Shaw alikuwa vizuri kweye vyumba vya kubadilishia nguo vya timu baada ya kuzimia uwanjani kufuatia kuumia kichwani wakati wa mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Hispania usiku wa jana.
  Beki huyo wa kushoto wa Manchester United aliumia wakati anagombea mpira wa juu na beki wa Real Madrid, Dani Carvajal katika dakika ya 46 England ikichapwa 2-1 Uwanja wa Wembley mjini London.
  Shaw alitibiwa kwa dakika sita na madaktari 10 uwanjani na kuwekewa oxygen hali ambayo ilizuwa wasiwasi mkubwa, ingawa Southgate alijaribu kuituliza kabla ya mchezaji mwenyewe kuondoa hofu kuwa kuposti maendeleo yake kwenye twitter.

  Luke Shaw akitibiwa na madaktari 10 baada ya kuzimia Uwanja wa Wembley jana 

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alicheza vizuri kabla ya kuumia na kuseti bao la timu yake, lililoffungwa na mchezaji mwenzake wa Man United, Marcus Ashford ambalo lilikuwa la kwanza mchezoni kabla ya wageni kutokea nyuma kushinda.
  Nafasi ya Shaw ilichukuliwa na Danny Rose dakika ya 52 huku akipelekwa vyumbani kwa matibabu zaidi mashabiki wakimpigia makofi na kumtakia heri.
  Kwa kuumia huko, Shaw atakosekana kwenye mchezo wa Jumanne usiku dhidi ya Uswisi Uwanja wa King Power. Kocha wake wa klabu, Mreno Jose Mourinho alikuwepo jukwaani akiushuhudia mchezo huo Uwanja wa Wembley. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAW: NINAENDELEA VIZURI NA NIPO KWEYE MIKONO SALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top