• HABARI MPYA

  Wednesday, September 19, 2018

  LIPULI YAPATA USHINDI WA KWANZA WA MSIMU LIGI KUU, YAWACHAPA VIBONDE ALLIANCE FC 1-0 SAMORA

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Lipuli ya Iringa imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibwaga Alliance FC kutoka mkoani Mwanza 1-0 katika mchezo wa mchana Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika ya sita na sasa Lipuli ya kocha Suleiman Abdallah Matola inafikisha pointi sita baada ya kutoa sare tatu mfululizo katika mechi zake za awali.
  Hali ni mbaya kwa Alliance FC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, kwani sasa inafikisha mechi tano bila ushindi, matokeo mazuri kwake yakiwa ni sare ya 1-1 ya African Lyon, tena nyumbani Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Lipuli ya Iringa imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI YAPATA USHINDI WA KWANZA WA MSIMU LIGI KUU, YAWACHAPA VIBONDE ALLIANCE FC 1-0 SAMORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top