• HABARI MPYA

  Sunday, September 16, 2018

  KIPCHOGE AWEKA REKODI MPYA YA DUNIA YA MARATHONI

  MWANARIADHA wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi mpya ya dunia kwenye mbio ndefu, Marathoni kwa kutumia saa mbili, dakika moja na sekunde 39 katika mbio za Berlin.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 ameipiku rekodi ya awali kwa zaidi ya dakika ya moja ambayo iliwekwa na Mkenya mwenzake, Dennis Kimetto aliyetumia Saa 2:02:57 mjini Berlin mwaka 2014.
  "Nakosa maneno ya kuzungumza katika siku hii," alisema Kipchoge. "Niko vizuri mno, nafurahi kuvunja rekodi ya dunia,".

  Mshindi wa mbio za wanawake ni Gladys Cherono wa Kenya pia aliyetumia muda wa Saa 2:18:11. Kipchoge anatambulika kama mmoja wa wanariadha wakubwa wa mbio ndefu wa muda wote.
  Alishinda mbio za London Marathon kwa mara ya tatu mapema mwaka huu na ni bingwa wa Olimpiki katika mbio hizo.
  "Ilikuwa vigumu," amesema Kipchoge. "Nakimbia mbio zangu mwenyewe, Nawaamini walimu wangu, programu zangu na kocha wangu. Hicho ndicho kinachonifanya nimalize kilomita,".
  Mwaka 2017, Kipchoge alikosa kwa sekunde 26 tu kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia Marathoni ndani ya saa mbili.
  Mkenya huyo alitumia muda wa Saa 2:00.25, lakini kwa sababu ya vipimo ambavyo havikuthibitishwa vilivyotumika, muda huo haukuhesabiwa kama rekodi ya dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPCHOGE AWEKA REKODI MPYA YA DUNIA YA MARATHONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top