• HABARI MPYA

  Thursday, September 13, 2018

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA SH. 7,000 SEPTEMBA 30 UWANJA WA TAIFA, TIKETI ZA ELEKTRONIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga SC utakaochezwa Septemba 30, 2018.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba kiingilio cha chini katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani.
  Ndimbo amesema kwamba katika jukwaa la VIP A watu wataingia kwa Sh. 30,000, VIP B na  C Sh 20, 000 na tiketi zitaanza kuuzwa Septemba 20,2018 kupitia Selcom.

  “Tunaomba watu wawahi kununua tiketi zao mapema kwa kupitia kadi ya Selcom ambayo inawapa urahisi wa kununua tiketi zao. Kadi za Selcom zinapatikana kwa mawakala waliopo sehemu mbalimbali nchini,” amesema.
  Wakati huo huo: Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajia kuendelea kesho Ijumaa Septemba 14,2018 kwenye Viwanja viwili.
  Kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga Azam FC watakuwa wageni wa Mwadui FC mchezo utakaochezwa saa 8 mchana.
  African Lyon wao watakuwa Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam kuwakaribisha Coastal Union kutoka Tanga mchezo utakaochezwa saa 10 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA SH. 7,000 SEPTEMBA 30 UWANJA WA TAIFA, TIKETI ZA ELEKTRONIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top