• HABARI MPYA

  Wednesday, September 19, 2018

  JUMANNE MSANGAA: BAJAJI YA SPORTPESA IMENIEPUSHIA MAISHA YA KUBANGAIZA KIJITONYAMA

  UKIFIKA maeneo ya Kijitonyama Heko, jina la kijana Jumanne Msangaa si geni masikioni mwa watu wanaishi maeneo haya.  
  Katika simulizi ya kusisimua kijana huyu anasema katika maisha yake yote alikuwa anazifanya shughuli ambazo zilikuwa zinamuingizia kipato kidogo sana. 
  Anaposimulia juu ya aina ya maisha aliyokuwa anaishi na jinsi alivyokuwa anahangaika kujiingizia kipato kisichokidhi maisha yake, anaonekana kutabasamu huku mkononi akiwa ameshika funguo ya bajaj mpya aina ya TVS king aliyoipata baada ya kubashiri na Sportpesa.  
  Jumanne Msangaa ni mmoja wa washindi wa mfano wa mafanikio ya kampeni ya Sportpesa  

  Wakati kampuni hii ya ubashiri wa michezo mbalimbali inapozungumzia juu ya kuinua maisha ya watu, simulizi ya kijana Jumanne inakuunganisha na msingi wa furaha yake aliyonayo iliyokuja kwa kufumba na kufumbua akiwezeshwa na Sportpesa. 
  Promosheni maalumu ya siku mia moja ya shinda na Sportpesa ambayo ilimwaga bajaj mpya takribani mikoa ishirini na mitatu nchi nzima, inatiliwa mkazo na simulizi za kusisimua za maisha yaliyobadilika ya washindi wa bajaj hizo ambapo kijana Jumanne Msangaa ni mmoja kati ya washindi wengi ambao ni mifano hai ya mafanikio ya kampeni ya Sportpesa ya kuinua na kuboresha maisha ya watu
  Hii inaonyesha uwezo wa vidole kucheza na *150*87# huku akili ikitafakari vyema matokeo ya mechi mbalimbali na namna washindi walivyofurahia mara mbili na furaha yao kukua na kuongezeka, kwa timu nzima ya ushindi Sportpesa ni zaidi ya rafiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUMANNE MSANGAA: BAJAJI YA SPORTPESA IMENIEPUSHIA MAISHA YA KUBANGAIZA KIJITONYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top