• HABARI MPYA

  Monday, September 10, 2018

  FEI TOTO AWAAHIDI YANGA UBINGWA, AOMBA APANGWE MECHI NA SIMBA SEPTEMBA 30 AWAONYESHE

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewaahidi mashabiki wa klabu yake, Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/2019.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Feisal amesema kwamba pamoja na kwamba mashabiki wa timu hiyo hawaipi nafasi yao kutamba mbele ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC lakini mwishoni mwa msimu watafurahi na roho zao.
  Feisal aliyetakata katika mchezo wa kirafiki jana dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Yanga ikiibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee Yussuf Mhilu dakika ya 84 amesema kwamba anajisikia vizuri sana pale anapoona kila anapopata mpira na kuucheza mashabiki wanashangalia, hivyo ahadi yake kubwa ni kuhakikisha anawapa ubingwa msimu huu.

  Feisal Salum ‘Fei Toto’ (kulia) amewaahidi Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

  "Ninajua mashabiki wa Yanga wanafurahia ninachokifanya na wana imani kubwa juu yangu. Na mimi ninafurahia hilo na pia najisikia vizuri. kikubwa ninachowaahidi ni ubingwa,” amesema Feisal aliyesajiliwa Julai kutoka JKU ya kwao, Zanzibar.
  Aidha, kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya mahasimu, Simba uliopangwa kuchezwa Septemba 30, kiungo huo ameahidi kufanya makubwa iwapo atapewa nafasi katika kikosi cha Yanga.
  “Simba na Yanga hizi zote ni timu nzuri, ninashindwa kusema nani ataibuka mshindi siku hiyo, yote anapanga Mungu, lakini ninawaambia mashabiki wa Yanga siku hiyo ni ushindi tu,”amesema kiungo huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO AWAAHIDI YANGA UBINGWA, AOMBA APANGWE MECHI NA SIMBA SEPTEMBA 30 AWAONYESHE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top