• HABARI MPYA

  Monday, September 17, 2018

  ESPERANCE YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, TUNIS
  TIMU ya Esperance ya Tunisia imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya ndugu zao, Etoile du Sahel Jumamosi Uwanja wa Olimpiki mjini Rades.
  Mabao ya wenyeji katika mchezo wa juzi yalifungwa na Chamseddine Dhaouadi dakika ya pili tu na Sameh Derbali dakika ya 77, wakati la Etoile lilifungwa na Ammar Jemal dakika ya 29. 
  Sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano Septemba 21 Uwanja wa Olimpiki wa mjini Sousse utawabeba Esperance hadi Nusu Fainali, wakati Etoile watatakiwa kushinda 1-0 tu kwenda Nane Bora.
  Mechi nyingine ya jana, Primiero de Agosto ililazimishwa sare ya 0-0 na mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe Uwanja wa November 11 mjini Luanda, Angola.
  Sasa Mazembe watakuwa na kazi nyepesi Ijumaa wiki hii kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi. 
  Mechi za Ijumaa, bao pekee la beki Msenegal, Isla Daoudi Diomande dakika ya 16 lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 ES Sétif dhidi ya mabingwa watetezi, Wydad Casablanca ya Morocco Uwanja wa Mei 8, 1945 mjini Setif, Algeria.
  Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Al Ahly ya Misri wakalazimisha sare ya 0-0 ugenini kwa Horoya Uwanja wa September 28 mjini Conakry, Guinea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ESPERANCE YABISHA HODI NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top