• HABARI MPYA

  Tuesday, September 18, 2018

  CAF YATAJA MAREFA WA MECHI ZOTE MBILI ZA TAIFA STARS NA CAPE VERDE PRAIA NA DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetaja waamuzi kutoka nchini Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo mjini Praia Oktoba 12,2018.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo amesema leo kwamba kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Drissa Kamory Niabe, Mwamuzi msaidizi namba 2 Baba Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.
  Aidha, mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti.

  Mwamuzi wa katikati atakuwa Souleiman Ahmed Djama na Mwamuzi msaidizi namba moja Farhan Bogoreh Salime, Mwamuzi msaidizi namba 2 Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.
  Kamishna wa mchezo anatokea Malawi Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda Michael Gasingwa.
  Wakati huo huo: CAF imewateua waamuzi kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 Cameroon kati ya Shelisheli na Afrika Kusini utakaochezwa Uwanja wa Stade Linite Oktoba  16,2018.
  Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Mfaume Ali Nassoro akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Ferdinand Chacha, Mwamuzi msaidizi namba 2 Alli Kinduru na Mwamuzi wa akiba Elly Sasii. Mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve. 
  Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limemteua Bwana Ahmed Idd Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, mchezo ambao utazikutanisha Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Kamuzu Stadium katika Mji wa Blantyre.
  Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini Waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe OmniSports Stade Des Martyrs Oktoba 13,2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YATAJA MAREFA WA MECHI ZOTE MBILI ZA TAIFA STARS NA CAPE VERDE PRAIA NA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top