• HABARI MPYA

  Saturday, September 08, 2018

  BIASHARA UNITED KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA SONY SUGAR YA KENYA MUSOMA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, MARA
  TIMU ya Biashara United ya Mara kesho itakuwa na mchezo wa kirafiki na wapinzani kutoka Kenya, Sony Sugar ambao utafanyika Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Mchezo huo ni maalum kukiweka sawa kikosi cha Biashara United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, kufuatia michuano hiyo kusimama wikiendi hii kupisha kalenda ya mechi za kimataifa.
  Na kocha Mnyarwanda Hitimana Thierry wa Biashara United anataka wachezaji wake wasibweteke kwa mapumziko haya ya wikiendi hii ndiyo maana ameomba mechi.

  Na uzuri zaidi kwake anapata mechi dhidi ya wapinzani kutoka Ligi Kuu ngumu ya nchi nyingine, Kenya ambayo itamsaidia kukiimarisha kikosi chake.
  Kwa sasa, Biashara United inayojivunia kiungo mshambuliaji mkongwe, Uhuru Suleiman Mwambungu imevuna pointi tat utu baada ya mechi tatu za Ligi Kuu, ikishinda moja na kufungwa mbili zote ugenini.
  Ilianza vyema Ligi Kuu kwa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Singida United Uwanja wa Namfua kabla ya kwenda kupigwa 1-0 mfululizo na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani na Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA SONY SUGAR YA KENYA MUSOMA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top