• HABARI MPYA

  Wednesday, September 05, 2018

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA ARUSHA UNITED MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imetoka sare ya bila kufungana na Arusha United ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
  Huo unakuwa mchezo wa pili wa kirafiki timu hiyo ikicheza bila kushinda, baada ya Jumamosi asubuhi kuchapwa mabao 2-1 na Transit Camp ya Daraja la Kwanza pia, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm alisema baada ya mechi hiyo kwamba timu imeathiriwa na kukosa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza waliopo timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mechi dhidi ya Uganda.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm (kulia) amesema sare imetokana na timu kukosa wachezaji wake muhimu

  Baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Julai 13, mwaka huu wakiifunga Simba SC 2-1, mabao yake yakifungwa na Shaaban Iddi Chilunda na Aggrey Morris dhidi ya moja la wapinzani wao lililofungwa na Meddie Kagere, Azam FC ikaenda kufanya vibaya kwenye ziara ya mechi za kirafiki Uganda.
  Ilitoka sare ya bao 1-1 na Express, 0-0 na URA na kufungwa mabao 4-2 na pili wa Ligi Kuu Uganda, KCCA, kanla ya kurejea nchini na kuanza vizuri Ligi Kuu ikishinda mechi zote mbili za mwanzo, 2-0 na Mbeya City na 3-0 na Ndanda FC, zote Uwanja wa Azam Complex. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA ARUSHA UNITED MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top