• HABARI MPYA

  Wednesday, August 08, 2018

  TIMU ZA MICHUANO YA CECAFA U-17 KUFUZU AFCON 2019 ZAANZA KUWASILI NA ZOEZI LA KWANZA NI VIPIMO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU zitakazoshiriki mashindano ya kufuzu fainali za Afrika U17 Kanda ya CECAFA zimeanza kuwasili nchini na kufanya vipimo vya afya na umri.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kwamba leo zoezi la vipimo linaendelea kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).
  Michuano hiyo inayojulikana kama CECAFA Zonal Qualification inatarajiwa kuanza Jumamosi na wenyeji, Serengeti Boys wakiwa chini ya kocha Oscar Milambo, wameweka kambi hosteli za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

  Serengeti wataingia kwenye michuano hiyo wakitoka kuchukua ubingwa wa michuano ya Kombe la CECAFA Challenge nchini Burundi mwezi Aprili, mwaka huu.
  Serengeti Boys ilitwaa Kombe la CECAFA Challenge U-17 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye fainali Aprili 29 Uwanja wa Ngozi mjini Bujumbura, Burundi, mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66.
  Ikumbukwe Somalia ilifika fainali ya michuano hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad baada ya kuwatoa Uganda, wakati Tanzania iliwatoa Kenya katika mechi za Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU ZA MICHUANO YA CECAFA U-17 KUFUZU AFCON 2019 ZAANZA KUWASILI NA ZOEZI LA KWANZA NI VIPIMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top