• HABARI MPYA

  Wednesday, August 08, 2018

  POGBA AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE MAN UNITED ANAKWENDA BARCELONA

  KIUNGO Paul Pogba amewaambia wachezaji wenzake wa Manchester United kwamba anataka kuondoka Old Trafford kuhamia Barcelona.
  Pogba amewafahamisha wachezaji wenzake hilo kiasi cha saa 48 zilizopita kwamba anataka kuuzwa, ikiwa ni miaka miwili tangu ajiunge tena United kutoka Juventus kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 89.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 inafahamika amemtumia ujumbe wa maandishi wa simu ya mkononi Ed Woodward, akimfahamisha Makamu Mwenyekiti huyo wa United dhamira yake ya kuondoka, ingawa klabu imekana hilo.

  Paul Pogba amewaambia wachezaji wenzake Manchester United anataka kuhamia Barcelona  

  United imeendelea kusistiza kwamba Pogba hauzwi, kiasi cha siku mbili kabla kikosi cha Jose Mourinho hakijaanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya England kwa kucheza na Leicester City. 
  Watakuwa wana muda mfupi sana wa kusajili mbadala wake kabla ya dirisha la usajili kufungwa England Alhamisi Saa 11:00 jioni.
  Sasa wanakabiliwa na changamoto ya kumbakiza mchezaji asiye na furaha ambaye anatarajiwa kulipwa mshahara wa Pauni Milioni 9.62 kwa msimu, pamoja na posho Pauni Milioni 3.78, au kumruhusu Pogba aingie kwenye majadiliano ya wazi na Barcelona. 
  Dirisha la usajili la Hispania halifungwi hadi mwisho wa mwezi huu.
  Inafahamika Pogba amekubaliana vipengele na vigogo wa Katalunya kwa mkataba wa thamani ya Pauni Milioni 89.5 kwa miaka zaidi ya mitano — mshahara wa Pauni Milioni 18 ambao ni sawa na Pauni 346,000 kwa wiki — huku wakala wake, Mino Raiola akilisimamia kidete suala la kuhamia Nou Camp.
  Raiola amezungumzia sakata hilo jana akisema: "Siwezi kufanya matangazo juu ya Paul. Unatakiwa uzungumze na Manchester United.’ Inafahamika kwamba Pogba anataka kucheza Hispania na akina Lionel Messi na mchezaji mwenzake wa zamani Juventus, Arturo Vidal, ambaye alijiunga na Barcelona wiki iliyopita.
  Ametokea kupuuzwa na maisha Man United chini ya Mourinho baada ya uhusianio baina yao kuharibika msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE MAN UNITED ANAKWENDA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top