• HABARI MPYA

  Friday, August 10, 2018

  MTIBWA SUGAR KUMENYANA NA KMC KESHO UWANJA WA BANDARI MAANDALIZI YA MECHI YA NGAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mtibwa Sugar kesho kitashuka katika dimba la Bandari jijini Dar es salaam kucheza dhidi ya KMC ya jijini Dar es Salaam. 
  Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, huku mchezo wa ufunguzi ukiwa Reha dhidi ya Transit Camp.
  Washindi wa michezo hiyo watacheza fainali siku ya Jumapili katika uwanja wa Bandari huku waliopoteza michezo hiyo wakicheza mshindi wa tatu . Mechi hizo zimeandaliwa na timu ya Reha Football Club ili kuadhimisha wiki ya Reha.

  Kwa Mtibwa mechi hizo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC Agosti 18, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Swabur amesema kwamba yanaendelea vizuri.
  Kwa sasa benchi la Ufundi la Mtibwa Sugar linaongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Mayanga, Kocha Mkuu Zubery Katwila na Kocha Msaidizi, Patrick Mwangata, ambaye pia ni kocha wa makipa wote wachezaji wake wa zamani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR KUMENYANA NA KMC KESHO UWANJA WA BANDARI MAANDALIZI YA MECHI YA NGAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top