• HABARI MPYA

  Tuesday, August 07, 2018

  KROENKE ATAKA KUJIMILIKISHA ARSENAL YOTE PEKE YAKE

  Stan Kroenke ametoa ofa ya kununua hisa zaidi za Arsenal katika dili ambalo litafanya thamani ya klabu iwe pauni Bilioni 1 


  MTIRIRIKO WA HISA ZA ARSENAL 

  KSE (inamilikiwa na Stan Kroenke) - hisa 41,743 (asilimia 67.09)
  Red and White Securities (Usmanov) - hisa 18,695 (asilimia 30.04
  Hisa nyingine - 1,781 (asilimia 2.87)
  JUMLA YA HISA - 62,219 
  BILIONEA Mmarekani, Stan Kroenke anataka kujimilikisha Arsenal yote, baada ya mwanahisa huyo mkuu wa klabu kutoa ofa ya Pauni Milioni 550 kununua hisa za Alisher Usmanov. 
  Kroenke ambaye tayari anamiliki asilimia 67 kupitia kampuni yake ya Kroenke Sports Enterprise group (KSE), anasubiri majibu ya Usmanov juu ya kununua asilimia 30 ya hisa za Mrusi huyo.
  Kroenke amesema katika taarifa yake kwenye soko la hisa la London kwamba anaamini klabu hiyo itanufaika ikiwa inamilikiwa naye binafsi na mwanawe wa kiume, Josh atapewa majumumu zaidi ya uendeshaji.
  Kroenke Jr anaweza akapewa nafasi ya kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu iwapo Ivan Gazidis ataamua kukubali ya AC Milan na kuondoka Arsenal. 
  Hiyo inakuwa mara ya pili kwa KSE kufanya jaribio hilo, baada ya Oktoba mwaka jana kutoa ofa ya kiasi cha Pauni Milioni 525 kutaka kununua hisa za Usmanov, lakini akakataliwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KROENKE ATAKA KUJIMILIKISHA ARSENAL YOTE PEKE YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top