• HABARI MPYA

  Friday, August 03, 2018

  GWIJI WA YANGA NA TAIFA STARS KENNY MKAPA ATEULIWA KUWA MENEJA WA SERENGETI BOYS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Kenneth ‘Kenny’ Pius Mkapa ameteuliwa kuwa Meneja wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kwamba Mkapa, beki hodari wa kushoto enzi zake, anaanza kazi mara akiungana na timu iliyopo kambini katika hosteli za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Serengeti ipo kambini inajiandaa kwa mechi za kufuzu fainali za Afrika kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, iitwayo CECAFA Zonal Qualification itakayoanza Agosti 11, mwaka huu.

  Beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Kenny Mkapa ameteuliwa kuwa Meneja wa Serengeti Boys 

  Serengeti wataingia kwenye michuano hiyo wakitoka kuchukua ubingwa wa michuano ya Kombe la CECAFA Challenge nchini Burundi mwezi Aprili, mwaka huu.
  Serengeti Boys ilitwaa Kombe la CECAFA Challenge U-17 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye fainali Aprili 29 Uwanja wa Ngozi mjini Bujumbura, Burundi, mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66.
  Ikumbukwe Somalia ilifika fainali ya michuano hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad baada ya kuwatoa Uganda, wakati Tanzania iliwatoa Kenya katika mechi za Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA YANGA NA TAIFA STARS KENNY MKAPA ATEULIWA KUWA MENEJA WA SERENGETI BOYS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top