• HABARI MPYA

  Friday, August 03, 2018

  CAF YAMTEUA REFA WA TANZANIA KUSHIRIKI KOZI YA WAAMUZI UGANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  REFA wa Tanzania, Soud Idd Lila ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF)kushiriki katika kozi ya Waamuzi Vijana wenye vipaji itakayofanyika Kampala,Uganda kuanzia Septemba 14,2018 mpaka Septemba 18,2018.
  Lila anaingia kwenye kipengele cha waamuzi wasaidizi. Septemba 13,2018 itakuwa siku ya kuwasili wakati ufunguzi utakuwa Septemba 14,2018.
  Kozi itahusisha jumla ya Waamuzi 40 ambapo Waamuzi 15 watakuwa wa katikati, Waamuzi wasaidizi 15 wakati upande wa waamuzi Wanawake Waamuzi 5 watakuwa waqkatikati na Waamuzi wasaidizi 5.

  Soud Lila ameteuliwa na CAF kushiriki katika kozi ya Waamuzi Vijana wenye vipaji mjiji Kampala kuanzia Septemba 14 

  Kozi hiyo pia itakwenda sambamba na upimaji wa afya kwa Waamuzi, Utimamu wa mwili na mtihani wa kiufundi, mwamuzi atakayeshindwa atarudishwa nyumbani hataruhusiwa kushiriki kozi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAMTEUA REFA WA TANZANIA KUSHIRIKI KOZI YA WAAMUZI UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top