• HABARI MPYA

    Friday, August 10, 2018

    AZAM FC YAKUTANA NA KIPIGO KIKALI UGANDA, YAFUNGWA 4-2 NA KCCA LUGOGO

    Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
    AZAM FC imepoteza mchezo wa kwanza leo katika ziara yake ya Uganda baada ua kuchapwa mabao 4-2 na wenyeji, KCCA Uwanja wa klabu hiyo uliopo eneo la Lugogo mjini Kampala, Uganda.
    Azam FC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm anayesaidiwa na mzalendo, Juma Mwambusi ilitangulia kwa mabao ya beki Aggrey Morris dakika ya tatu na mshambuliaji mpya, Daniel Lyanga dakika ya sita.
    Lakini KCCA wakazinduka na kusawazisha mabao hayo ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Muzamil Mutyaba dakika ya 15 na Timoth Awanyi dakika ya 44, kabla ya kuongeza mengine mawili kipindi cha pili kupitia kwa Allan Kyambadde dakika ya 48 na Patrick Kaddu dakika ya 69.

    Huo ulikuwa ni mchezo wa pili katika kambi yake ya Uganda kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya awali kulazimishwa sare ya 0-0 na URA Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAKUTANA NA KIPIGO KIKALI UGANDA, YAFUNGWA 4-2 NA KCCA LUGOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top