• HABARI MPYA

  Tuesday, July 10, 2018

  YANGA SC YAMSAJILI MO BANKA WA MTIBWA SUGAR MIAKA MIWILI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mohammed Issa 'Banka' amejiunga na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  'Mo Banka' ametambulishwa leo Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh aliyeambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam.
  Nyika amesema kwamba Mohamed Issa 'Banka' ni mchezaji mzuri na wameridhika na kiwango chake ndio maana wamemsajili na kumpatia mkataba wa miaka miwili.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh akimkabidhi jezi kiungo wa timu hiyo, Mohammed Issa 'Banka' 
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh (kushoto) akiwa na kiungo mpya, Mohammed Issa 'Banka' na Mwenyekiti wa Usajili, Hussein Nyika 

  "Mohamed Banka ni mchezaji mzuri tumemfuatilia kwa undani zaidi tangu akiwa Mtibwa Sugar na tutamsikiliza mwalimu kama atamchukua ashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika au la ila kuanzia sasa Mohamed Banka ni mali ya Klabu ya Yanga "amesema Nyika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMSAJILI MO BANKA WA MTIBWA SUGAR MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top