• HABARI MPYA

  Monday, July 09, 2018

  WAGENI WA LIGI KUU BIASHARA UNITED WAPATA KATIBU MKUU ANAITWA HAJI MTETE

  Na Mwandishi Wetu, MARA
  KLABU ya Biashara United ya Mara imemtangaza Haji Mtete kuwa Katibu Mkuu wake kuanzia sasa ili kukidhi sifa zinazotakiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa klabu za Ligi Kuu, ambayo mojawapo ni kuwa na Sekretarieti.
  Lakini pia Mwenyekiti wa klabu hiyo, Suleiman Mataso amesema kwamba baada ya muda mrefu wa klabu kutokuwa na Mtendaji Mkuu wamelazimika pia kufanya uteuzi huo.
  Amesema kwamba kwa kukosa Mtendaji Mkuu rasmi wa klabu, ilisababisha mambo mengine kutokamilika kwa wakati.

  Mwenyekiti wa Biashara United, Suleiman Mataso (katikati) akimtambulisha Haji Mtete (kushoto) kuwa Katibu Mkuu wa klabu leo

  "Tumekuwa na shida sana kwa kutokuwa na Katibu mkuu hatua ambayo mambo mengine yakikuwa yanakwama" alisema Mwenyekiti hiyo
  Kwa upande wake, Katibu Mkuu huyo wa klabu hiyo, Mtete ameshukuru uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi hiyo na kusema atatumia nafasi hiyo kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
  "Kwanza mimi ninashukuru kwa uamuzi huu wa uongozi wa timu ya Biashara United (Mara) kunipa nafasi hii na naamini nitasaidiana na viongozi wengine kuhakikisha msimu huu tunafanya vizuri katika ligi kuu Tanzania Nara"alisema Mtete
  Haji Mtete amewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Musoma kwa kipindi cha miaka nane na katika wa chama cha Makocha mkoani humo kwa miaka mitatu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAGENI WA LIGI KUU BIASHARA UNITED WAPATA KATIBU MKUU ANAITWA HAJI MTETE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top