• HABARI MPYA

  Thursday, July 12, 2018

  SINGIDA UNITED YAIZIDI KETE YANGA TENA, YAMSAJILI ‘FEI TOTO’ MIAKA MITATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kutolewa katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Singida United imeimarisha kikosi chake kwa kumsajili kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka JKU ya Zanzibar aliyekuwa anatajwa pia kuwaniwa na vigogo, Yanga SC. 
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Zanzibar amesaini mkataba wa miaka mitatu.
  Sanga amesema kwamba Fei alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa JKU, lakini walizungumza na klabu yake na kufikia makubaliano ya kuununua mkataba huo. 

  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo akimkabidhi jezi ya timu hiyo kiungo Feisal Salum baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka JKU 

  Huu ni usajili wa pili Singida United inafanya tangu iwe chini ya kocha Mzanzibari, Hemed Suleman ‘Morocco’, baada ya kipa, David Kisu kutoka Njombe Mji FC.
  Singida United imemsajili Fei Toto baada ya kuvutiwa naye akiichezea JKU katika Kombe la Kagame. Na Fei ndiye aliyeisaidia JKU kuitoa Singida katika Robo Fainali ikishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAIZIDI KETE YANGA TENA, YAMSAJILI ‘FEI TOTO’ MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top